Si hali nyingi ambazo hupata umakini mkubwa—na mabishano—kama ugonjwa wa spektra wa usonji (ASD), haswa kati ya wazazi na watoto wachanga. Watu walio na ASD wana ugumu wa kuendeleza mahusiano ya kawaida ya kijamii, hutumia lugha kwa njia isio ya kawaida au hawaitumii kabisa na huonyesha tabia za kuzuia na zinazo jirudiarudia. Wanaweza kuwa na wakati mgumu kuelewa ishara za kijamii au kuwaza kile ambacho watu wengine wanaweza kuwa wanafikiria, hali ambayo inaweza kufanya maingiliano ya kijamii kuwa na changamoto.
Kwa sababu ni spektra, watu walio na ASD hupata dalili mbalimbali na tatizo hilo huathiri maisha yao katika njia tofauti. Matokeo yake, ASD inakabiliwa na dhana zisizo za kweli na ukosefu wa uelewa kwa kiasi kikubwa, chanzo chake na jinsi inavyoathiri watu katika awamu mbalimbali za maisha yao. Hapa kuna dhana saba zisizo za kweli kuhusu usonji na kile ambacho watu walio na usonji na wale ambao wanawasaidia wanahitaji kukifahamu.
Dhana #1: Ni wavulana pekee ndio hupata usonji
ASD hutokea kwa takriban mtu 1 kati ya 36 nchini Marekani na wavulana wana uwezekano wa kuipata mara nne zaidi kuliko wasichana. Lakini wasichana wanaweza kupata ASD. Hali nyingine ambayo wazazi wanapaswa kufahamu ni ugonjwa wa Rett, ambao hutokea zaidi kwa wasichana kuliko wavulana. Ugonjwa wa Rett una sifa nyingi sawa na zile za ASD, na pia utofauti mkubwa. Kimahususi, karibu watu wote walio na ugonjwa wa Rett kwa kawaida huwa na ulemavu wa akili.
Dhana #2: Watu wote walio na ASD pia wana ulemavu wa akili
Ulemavu wa akili na ASD sio sawa Ulemavu wa akili hutokea zaidi kwa watu walio na ASD, lakini sio kila mtu aliye na ASD ana ulemavu wa akili na sio kila mtu aliye na ulemavu wa akili ana ASD. Tatizo la upungufu wa umakini/kukosa utulivu (ADHD) ni hali nyingine ambayo mara nyingi—lakini si kila wakati—inapishana na ASD.
Dalili ambazo zinalingana na hali hizi kwa kawaida huwa za kuonekana baadaye kidogo katika maisha. Kwa wazazi, ishara ya kwanza ya kuangalia ni kuchelewa katika maendeleo ya uwezo wa kutumia lugha. Viashiria vingine vya mapema ni pamoja na tabia za kurudia, hitaji la mazoea na utofauti katika uchakataji wa fahamu kwa vitu kama kelele, mwangaza na umbile. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa mambo haya yanaweza kuwa ishara za hali mbalimbali. Na kwa watoto wengi, ishara hizi sio ishara za tatizo lolote la kiafya.
Dhana #3: Watu wazima na watoto wenye udadisi huwa na ASD
Neno "kwenye spektra" limekuwa ufupisho wa kufafanua mtu ambaye anaweza kuwa na aibu kidogo, asiye na ustadi wa kijamii au asiyevutiwa sana na mada fulani. Watu hawa mara nyingi huwa hawana ASD.
Utamaduni wa Pop mara nyingi hueleza watu walio na usonji kama watu wenye talanta—werevu zaidi kwenye muziki au wenye kipaji cha hisabati. Baadhi ya watu walio na ASD wana ujuzi wa kipekee, lakini huwa hawana nguvu zisizo za kawaida. Ni bora zaidi kutokuchukulia ASD kama "tatizo" na kuichukulia kama "utofauti." Wakati mwingine tofauti hizo zinaweza kuwa na usaidizi katika hali fulani, lakini sisi wote ni watu ambao tuna maumbile na uwezo wetu wenyewe wa kipekee.
Wakati huo huo, utambuzi wa ASD unaweza kuwa zana bora zaidi kwa watu binafsi na familia. Hakuna vipimo vya maabara vya kutambua ASD. Badala yake, inategemea uwepo wa hali mbalimbali. Utambuzi huu unaweza kuwa ni wenye msaada mkubwa huku wazazi wakitafuta huduma na suluhisho ili kupata usaidizi unaohitajika kwa watoto wao, ikiwa ni pamoja na tiba ya kuzungumza, tiba ya shughuli za kila siku na mengine zaidi.
Dhana #4: Ni watoto pekee ndio hupata ASD
Mtu hubaki na ASD katika maisha yake yote na athari ya hali hii hubadilika kwa kadiri mtu anavyozidi kukua. Watu wenye ASD hujifunza kuzoea hali za kijamii ambazo hubadilika kwa kadiri wanavyozidi kukua, ikiwa ni pamoja na nyakati za ujana na kuingia katika maeneo yao ya kazi pale wanapoweza kufanya hivyo. Eneo moja ambalo watu wazima wenye umri mdogo walio na ASD mara nyingi wanahitaji usaidizi ni katika matumizi ya mfumo wa huduma za afya. Mara nyingi, watu watahama kutoka kwa daktari wa watoto hadi kwa mtaalam wa tiba na magonjwa ya akili ili kuendelea na matibabu na dawa wakati wanapoelekea kwenye utu uzima.
Dhana #5: Hakuna tiba ya ASD
Bado madaktari hawajagundua chanzo cha ASD. Tunajua kuwa mara nyingi hutokea kwa wanandugu na jamaa, lakini inaweza kuathiri kila mwanafamilia kwa njia tofauti. Ni ukweli kuwa kwa watu waliotambuliwa kuwa na ASD, hakuna matibabu mahususi ambayo madaktari wanapendekeza. Lakini, kuna njia kadhaa zilizothibitishwa za kusaidia watu kuboresha maisha yao, ikiwa ni pamoja na mbinu zinazotegemea hali ya kitabia na dawa ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti wasiwasi na mihemko ya ghafla ya kitabia. Watu walio na ASD mara nyingi hunufaika kutokana na mazoezi ya kufanya mazungumzo au "miongozo" ya kuwaongoza wanapokuwa katika mazingira ya kijamii.
Mara nyingi, wazazi watatafuta matibabu mbadala ya watoto walio na ASD. Baadhi ya njia hizi za kukabiliana na hali hii zinaweza kuwa na madhara. Ni muhimu kuzijadili na daktari kwanza na kujaribu jambo moja baada ya lingine ili kuhakikisha kuwa unaelewa athari iliyonayo njia fulani ya kukabiliana na hali.
Dhana #6: Chanjo husababisha ASD
Chanjo haisababishi ASD. Kuna tafiti nyingi za kiwango cha juu zinazoonyesha kwamba hakuna uhusiana baina ya vitu hivi viwili. Sababu moja ambayo inaweza kuwa ndio chanzo cha dhana hii ni kwamba wazazi wengi wanaanza kutambua dalili za ASD katika wakati ule ule ambao watoto wao wanaanza kupata chanjo za magonjwa mbalimbali. Licha ya utukizi huu, ni muhimu watoto wapokee chanjo zinazohitajika ili kujikinga na kuwakinga wengine kutokana na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Dhana #7: ASD inasababishwa na malezi mabaya
Kwa miongo kadhaa, tumejua kuwa "malezi mabaya" hayachangii au kusababisha ASD. Wazazi na walezi huwa na wajibu mkubwa katika kuwasaidia watoto wao kufanikiwa na wana wajibu mkubwa katika namna ambavyo watoto wao wanashughulika na ulimwengu, lakini matendo yao huwa hayasababishi ASD.
Kama ilivyo kwa kila mmoja wetu, kila mtu aliye na ASD ni wa kipekee. Tunapokutana na watu walio na ASD mahali walipo na kupata njia za kuungana nao, huwa tunafanya vyema zaidi.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu Ugonjwa wa Spektra wa Usonji, tembelea ukurasa wa Miongozo au Vidokezo vya Haraka kuhusu mada hii.